LIONEL MESSI NI NANI ?
Lionel messi ni mchezaji wa kimataifa wa argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya huko hispania, Anafahamika sana kwa jina hilo , lakini jina lake kamili ni Lionel andres messi , na alizaliwa mnamo juni 24 mwaka 1987 huko Rosario, argentina. Alikulia na kuanza kucheza soka nchini kwao argentina katika klabu ya Newell"s old boys , mpaka alipotimiza umri wa miaka 13 ndipo alipochukuliwa na klabu ya FC Barcelona.
MESSI ALIFIKAJE FC BARCELONA ?
katika maisha yake ya utotoni, messi alikumbwa na tat izo la upungufu wa homoni ya ukuaji, jambo ambalo lingepelekea kupunguza kasi ya ukuaji wake. kutokana na umaskini , familia yake ilishindwa kugharamia matibabu yake, lakini kipaji chake kilichoonwa na maskauti wa fc barcelona, kilisaidia kufanyika makubaliano kati ya familia yake na klabu hiyo, na hatimaye ikabidi messi aende nchini hispania kujiunga na FC Barcelona ambako angetibiwa tatizo lake pamojha na kucheza soka katika klabu hiyo , hii ilikuwa mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 13.
MAISHA YA AWALI KATIKA FC BARCELONA
Lionel messi aliingia katika akademi ya FC Barcelona ,maarufu ka,ma "La masia" ambako aliendeleza kipaji chake cha soka. Messi alizichezea timu za vijana za FC Barcelona katika ngazi zote,kwenye kipindi cha mwaka 2000 hadi 2004.
Na hatimaye mnamo oktoba mwaka 2004 alifanikiwa kuichezea kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa ya FC Barcelona. Tangia hapo aliweza kuendelea kucheza timu ya wakubwa katika misimu iliyofuatia, huku akizidi kuongeza kiwango chake .
Taratibu akaanza safari yake ya mafanikio msimu wa 2007/08, alipofanikiwa kuingia katika 3 bora katika tuzo ya mchezaji bora wa dunia , akiwa pamoja na Cristiano ronaldo na mshindi Ricardo kakla.
MAFANIKIO MAKUBWA NDANI YA FC BARCELONA
Hatimaye baada ya kufanikiwa kuingia 3 bora ya wachezaji bora duniani katika msimu wa 2007/08 , njia ya mafanikio kwa Lionel messi ilianza kufunguka ,kwani aliendeleza makali yake na kupata mafanikio makubwa katika misimu iliyofuatia.
Alifanikiwa kunyakua kwa mara ya kwanza tuzo ya mchezaji bora wa dunia , katika msimu wa 2008/09. Baada ya hapo messi aliweza kuibeba tena tuzo hiyo kwa mara 4 mfululizo. Hii ilikuwa katika misimu ya 2008/09 , 2009/10 , 2010/11 .na 2011/12.
Katika kipindi hicho aliisaidia FC Barcelona kushinda mataji mbalimbali kama vile ubingwa wa hispania ( la liga), kombe la uefa , kombe la mfalme na mataji mengine mengi.
Pia alifanikiwa kuweka rekodi mbalimbali kama vile kufunga magoli mengi ndani ya mwaka (91), baadhi ya rekodi hizi utaziona katika sehemu inayofuatia.
Na kata msimu wa 2014/15 , messi akishirikiana vizuri na Neymar pamoja na Luis suarez waliiwezesha FC Barcelonas kubeba makombe 3 kwa msimu ( "treble"), ukiwa ubingnwa wa ligi ,uefa na kombe la mfalme.
Hii ikamsaidia Lionel messi kushinda tena kwa mara ya 5 ,tuzo ya mchezaji bora wa dunia ( ballon d'or ), na hivyo kuweka rekodi ya kipekee kabisa.
Mpaka sasa ameichezea barcelona jumla ya mechi 563 na kuifungia magoli 464.
TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA
Katika timu ya taifa ya argentina, messi ameicheza katika ngazi za vijana mpaka watu wazima. Alikuwepo katika kikosi cha Argentina kilichoshinda medali ya dhahabu, katika mashinndano ya olimpiki ya mwaka 2008.
Alitoa msaada kwa timu yake ya taifa pia katika masindano ya kombe la dunia na copa america. Katika mwaka 2014 aliiwezesha argentina kufika fainali ya kombe la dunia, lakini walipoteza ka kufungwa bao 1 bila.Ameweza kuchaguliwa kama mchezaji bora wa mashindano, katika kombe la dunia mwaka 2010 na 2014.
Mpaka sasa ameichezea timu ya taifa jumla ya mechi 132 na kufunga magoli 69.(haijumuishi mechi za copa america zinazoendelea sasa hivi )
Katika upande huu , Lionel messi pamoja na mchumba wake Antonella roccuzo wamejaliwa kupata watoto 2.
Watoto hao ni TIAGO aliyezaliwa 2012 na MATEO aliyezaliwa 2015.
REKODI 5 BORA ZA LIONEL MESSI
- Ndiye mchezaji anayeongoza kwa kutwaa mara nyingi zaidi tuzo ya mchezaji bora wa dunia ( "Ballon d'or ") akiwa ameitwaa mara 5.
- Ni mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi ndani ya mwaka mmoja ( magoli 91, mwaka 2012)
- Ni mchezaji mwenye magoli mengi zaidi katika El clasico ( magoli 21 )
- Ni mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga magoli 200 katika la liga. (akiwa na miaka 25)
- ni mchezaji aliyetwaa kwa mfululizo zaidi tuzo ya Ballon d'or (mara 4)
Huyo ndiye Lionel andres messi , ambaye kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akishindanishwa na Cristiano ronaldo kutafuta mfalme wa soka wa dunia kwa sasa,
Je wewe kwa maoni yako, yupi bora kuliko mwenzake ?? usisahau kutoa maoni yako kuhusu hili.
Pia unaweza kutaja mchezaji ambaye ungependa na yeye afanyiwe uchanbuzi kama hivi, ili aweze kufahamika vizuri miongoni mwa mashabiki wa soka.
TUKUTANE KATIKA MAKALA IJAYO.............AHSANTE.
No comments:
Post a Comment