Utamjua Cristiano ronaldo kuanzia safai yake ya soka, klabu mbalimnali alizopitia na mafanikio aliyoyapatakupitia soka. karibu twende pamoja katika makal hii mwanzo mpaka mwisho.
CRISTIANO RONALDO NI NANI ?
Cristiano ronaldo am,baye jina lake kamili ni Cristiano ronaldo dos santos aveiro , ni mchezaji wa kimataifa wa ureno ambaye sasa anaichezea klabu ya Real madrid.
Alizaliwa mnamo tarehe 5 februari mwaka 1985, huko madeira, URENO. Ni mtoto wa mwisho wa Jose dinos aveiro na Maria dolores dos santos aveiro.
Alipewa jina la Ronaldo kama heshima kwa aliyekuwa raisi wa marekani, Ronald reegan aliyekuwa kipenzi cha baba yake ronaldo.
SAFARI YA MWANZO KATIKA SOKA.
Cristiano ronaldo alianza kucheza soka katika timu za mtaani kama vile Andorinha pamoja na Nacional.
Mnamo mwaka 1997, akiwa na miaka 12 alienda kufanya majaribio katika klabu ya Sporting lisbon.Aifanya majaribio hayo kwa siku 3, na baada ya klabu hiyo kuridhishwa na kiwango chake ikaamua kumsajili kwa bei ya euro 1500.
Aliendelea kucheza katika klabu hii ambapo mpaka mwaka 2003, aliichezea jumla ya mechi 25 na kufunga mabao 3.
Kartika maka 2003, Ronaldo alionyesha kiwango cha juu kwenye mechi ya kirafiki kati ya Manchester united na Sporting lisbon. Aliisaidia klabu yake kushinda 3-1, lakini kiwango chake kliwakosha wachezaji wa Man u, wakamsihi sir. Alex ferguson amsajili Cristiano ronaldo.
Hatimaye akiwa na umri wa miaka 18, Cristiano ronaldo alisajiliwa na Manchester united kwa ada ya pauni milioni 12.
MAISHA KATIKA MANCHESTER UNITED
Alipotua Man united, ronaldo aliomba apewe jezi namba 28 lakini akapewa jezi namba 7. Ambayo ilikuwa imevaliwa na magwiji wa Man united kama vile George best, Eric cantona na David beckham. Hii ikawa chachu kwa Ronaldo kujituma zaidi katika soka.
Alicheza mechi yake ya kwanza Man u mnamo agosti 16 mwaka 2003, hii ilikuwa mechi dhidi ya Bolton wanderers ambayo iliisha kwa man u kushinda 4-0.
Aliifunga goli lake la kwanza Man united kwa faulo , katika mechi dhidi ya Portsmouth ambayo Man united walishinda 3-0. Aliendelea kucheza kwa juhudi zaidi katika kikosi cha Man united .
Mafanikio katika Man united
Ronaldo alfunga magoli 2 yake ya kwanza katika ligi ya mabingwa ulaya msimu wa 2006/07, katika ushindi wa 7-1 wa man u dhidi ya As roma.
Alishinda pia taji lake la kwanza la ubingwa wa England (EPL) msimu wa 2006/07.
Ronaldo alifunga hat-trick yake pekee MAan united katika mechi dhidi ya newcastle,akiisaidia Man united kushinda 6-0 , mwaka 2008.
Katika msimu wa 2007/08 pia allfunga jumla ya mabao 42, akawa mfungaji bora wa EPL huku akiiwezesha Man united kubeba ubingwa wa ligi kuu uingereza pamoja na taji la ligi ya mabingwa ulaya.
Hii ikamsaiodia kuweza kushinda tuzo za mchezaji bora wa ulaya na mchezaji bora wa dunia kwa msimu huo.
Msimu wa 2008/09 ulikuwa ni msimu wa mwisho kwa Cristiano ronaldo katika klanu ya Manchester united, kwani msimu uliofuatia aliuzwa kuelekea Real madrid.
Kwa ujumla akiwa Man united, Ronaldo alicheza jumla ya mechi 196 na kufunga magoli 84.
MAISHA NDANI YA REAL MADRID.
Mnamo mwaka 2009, Cristiano ronaldo alijiunga na klabu ya Real madrid kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia kwa kipindi hicho. Aliuzwa kwa pauni milioni 80 kutoka Man united kuelekea Real madrid.
Aliicheza mechi yake ya kwanza Real madrid dhidi ya Deportivo la coruna mnamo agosti 29 mwaka 2009, na akafanikiwa kufunga bao kwa mkwaju wa penati, Aliweza kufanikiwa kufunga tena katika mechi 4 zilizofuatia.
Mafanikio ndani ya Real madrid
Katika msimu wa 2011/12 , ronaldo alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 60 katika mashindano yote,na kuiwezesha Real madrid kushinda ubingwa wa La liga.
Cristiano ronaldo alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia msimu wa 2012/13, mara ya kwanza akiwa na Real madrid.
Pia msimu wa 2013/14 aliiwezesha Real madrid kushinda taji la 10 ("la decima") la lgi ya mabingwa ulaya (UCL) , huku yeye akiweka rekodi ya kufunga mabao 17 katika mashindano hayo.
Hii ikamsaidia kushinda tena tuzo ya mchezaji bora wa dunia " ballon d'or" , mara ya pili akiwa na Real madrid na mara 3 kwa ujumla.
Pia katika msimu wa 2015/16 , Cristiano ronaldo allisaidia klabu yake ya Real madrid kushinda taji la 11 la ligi ya mabingwa ulaya .
Katika mechi ya fainali dhidi ya Atletico madrid,, ronaldo ndiye aliyepiga penati ya ushindi kwa Real madrid.
Mpaka sasa ronaldo amecheza jumla ya mechi236 na kufunga magoli 260.
TIMU YA TAIFA YA URENO
Katika timu ya taifa, Cristiano ronaldo amekuwa na mchango mkubwa sana, na sasa ndiye kapteni wa timu ya taifa ya ureno.
Ameiwakilisha ureno katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2006, 2010 ma 2014.
Anakumbukwa kwa kuisaidia ureno kufuzu kombe la dunia 2014, katika mechi ya mtoano dhidi ya sweeden, ambayo alifunga mabai 3 ( hat-trick) yaliyoisaidia Urenio kushinda 3-2, hivyo kupata nafasi ya kushiriki kombe la dunia 014.
Mpaka sasa ameshaichezea timu ya taifa mechi 126 na kufunga magoli 56 ( kabla ya mashindano ya EURO 2016 ).
REKODI 5 BORA ZAIDI ZA CRISTIANO RONALDO
- Ni mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya ( magoli 17, 2013/14)
- Ni mchezaji mwenye hat-tricks nyingi zaidi katika msimu mmoja wa UEFA champions league ( hatricks 3, 2015/16 )
- Ni mchezaji pekee aliyeweza kufunga zaidi ya magoli 30 kwa msimu,kwa misimu 6 mfululizo ya La liga
- Ni mchezaji aliyefunga magoli mengi katika hatua ya makundi ya UEFA champions league ( magoli 11, 2015/16 )
- Ni mchezaji mwenye hat-tricks nyingi zaidi katika historia ya Real madrid ( 37)
Cristiano ronaldo pia ni balozi wa makampuni mbalimbali kama vile NIKE. Na amekuwa akifanya matangazo mbalimbali na kampuni hizo,
Pia Ronaldo ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Cristiano ronaldo jr.
Naam ndugu msomaji , huyo ndiye Cristiano ronaldo. Ni mchezaji nyota na aliyepata mafanikio makubwa katika soka,na hiyo ndiyo safari yake kuanzia mwanzo mpaka alipofikia sasa,
TUKUTANE KATIKA MAKALA IJAYO......AHSANTE
No comments:
Post a Comment