Friday, 9 September 2016

MAISHA YA UJANA

Aisee maisha haya yamejaa changamoto nyingi sana, kama kijana unapaswa uishi ukifahamu ya kwamba:-
* Muda ulionao unapaswa kutumiwa vizuri ili uweze kupata maendeleo katika maisha yako.

* Thubutu kuwa na ndoto katika maisha yako, hii itakusaidia kuweza kujua unataka nini katika maisha haya na sio kuishi kama bendera inayofuata upepo.

* Jifunze kutoka kwa watu wanaokuzunguka na vyanzo mbalimbali vya taarifa kama vile intaneti na vitabu .

* Usikate tamaa pale utakapofanya jambo na lisifanikiwe, kumbuka hata facebook unayoitumia wewe leo isingekua hapo ilipo kama sio moyo wa kusonga mbele alionao Mark zuckerberg.

     to be continued....

Sunday, 19 June 2016

HUYU NDIYE CRISTIANO RONALDO

Cristiano ronaldo ni jina la mwanasoka ambalo si geni miongoni mwa karibu mashabiki wote wa soka.Ni mchezaji aliyepata mafanikio makubwa sana katika ulimwengu wa soka, na katika makala hii utaenda kumjua zaidi mchezaji huyu.
Utamjua Cristiano ronaldo kuanzia safai yake ya soka, klabu mbalimnali alizopitia na mafanikio aliyoyapatakupitia soka. karibu twende pamoja katika makal hii mwanzo mpaka mwisho.

 CRISTIANO RONALDO NI NANI ? 
Cristiano ronaldo am,baye jina lake kamili ni Cristiano ronaldo dos santos aveiro , ni mchezaji wa kimataifa wa ureno ambaye sasa anaichezea klabu ya Real madrid.
Alizaliwa mnamo tarehe 5 februari mwaka 1985, huko madeira, URENO. Ni mtoto wa mwisho wa Jose dinos aveiro na Maria dolores dos santos aveiro.
Alipewa jina la Ronaldo kama heshima kwa aliyekuwa raisi wa marekani, Ronald reegan aliyekuwa kipenzi cha baba yake ronaldo. 


  SAFARI YA MWANZO KATIKA SOKA. 
Cristiano ronaldo alianza kucheza soka katika timu za mtaani kama vile Andorinha pamoja na Nacional.
Mnamo mwaka 1997, akiwa na miaka 12 alienda kufanya majaribio katika klabu ya Sporting lisbon.Aifanya majaribio hayo kwa siku 3, na baada ya klabu hiyo kuridhishwa na kiwango chake ikaamua kumsajili kwa bei ya euro 1500.
Aliendelea kucheza katika klabu hii ambapo  mpaka mwaka 2003, aliichezea jumla ya mechi 25 na kufunga mabao 3.
Kartika maka 2003, Ronaldo alionyesha kiwango cha juu kwenye mechi ya kirafiki kati ya Manchester united na Sporting lisbon. Aliisaidia klabu yake kushinda 3-1, lakini kiwango chake kliwakosha wachezaji wa Man u, wakamsihi sir. Alex ferguson amsajili Cristiano ronaldo.
Hatimaye akiwa na umri wa miaka 18,  Cristiano ronaldo alisajiliwa na Manchester united kwa ada ya pauni milioni 12.
                 



  MAISHA KATIKA MANCHESTER UNITED 
 Alipotua Man united, ronaldo aliomba apewe jezi namba 28 lakini akapewa jezi namba 7. Ambayo ilikuwa imevaliwa na magwiji wa Man united kama vile George best, Eric cantona na David beckham. Hii ikawa chachu kwa Ronaldo kujituma zaidi katika soka.
Alicheza mechi yake ya kwanza Man u mnamo agosti 16 mwaka 2003, hii ilikuwa mechi dhidi ya Bolton wanderers ambayo iliisha kwa man u kushinda 4-0.
Aliifunga  goli lake la kwanza Man united  kwa faulo , katika mechi dhidi ya Portsmouth ambayo Man united walishinda 3-0. Aliendelea kucheza kwa juhudi zaidi katika kikosi cha Man united .

       Mafanikio katika Man united
Ronaldo alfunga magoli 2 yake ya kwanza katika ligi ya mabingwa ulaya msimu wa 2006/07, katika ushindi wa 7-1 wa man u dhidi ya As roma.
Alishinda pia taji lake la kwanza la ubingwa wa England (EPL) msimu wa 2006/07.  
Ronaldo alifunga hat-trick yake pekee MAan united katika mechi dhidi ya newcastle,akiisaidia Man united kushinda 6-0 ,  mwaka 2008.
Katika msimu wa 2007/08 pia allfunga jumla ya mabao 42, akawa mfungaji bora wa EPL huku akiiwezesha Man united kubeba ubingwa wa ligi kuu uingereza pamoja na taji la ligi ya mabingwa ulaya.
Hii ikamsaiodia kuweza kushinda tuzo za mchezaji bora wa ulaya na mchezaji bora wa dunia kwa msimu huo.  
Msimu wa 2008/09 ulikuwa ni msimu wa mwisho kwa Cristiano ronaldo katika klanu ya Manchester united, kwani msimu uliofuatia aliuzwa kuelekea Real madrid.
Kwa ujumla akiwa Man united, Ronaldo alicheza jumla ya mechi 196 na kufunga magoli 84. 

        



   MAISHA NDANI YA REAL MADRID.  
Mnamo mwaka 2009, Cristiano ronaldo alijiunga na klabu ya Real madrid kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia kwa kipindi hicho. Aliuzwa kwa pauni milioni 80 kutoka Man united kuelekea Real madrid.
Aliicheza mechi yake ya kwanza Real madrid dhidi ya Deportivo la coruna mnamo agosti 29 mwaka 2009, na akafanikiwa kufunga bao kwa mkwaju wa penati, Aliweza kufanikiwa kufunga tena katika mechi 4 zilizofuatia.

         Mafanikio ndani ya Real madrid  
Katika msimu wa 2011/12 , ronaldo alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 60 katika mashindano yote,na kuiwezesha Real madrid kushinda ubingwa wa La liga. 
Cristiano ronaldo alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia msimu wa 2012/13, mara ya kwanza akiwa na Real madrid.
Pia msimu wa 2013/14 aliiwezesha Real madrid kushinda taji la 10 ("la decima")  la lgi ya mabingwa ulaya (UCL) , huku yeye akiweka rekodi ya kufunga mabao 17 katika mashindano hayo.
Hii ikamsaidia kushinda tena tuzo ya mchezaji  bora wa dunia " ballon d'or" , mara ya pili akiwa na Real madrid na mara 3 kwa ujumla.
   
 
     
 
 
    Pia katika msimu wa 2015/16 , Cristiano ronaldo allisaidia klabu yake ya Real madrid kushinda taji la 11 la ligi ya mabingwa ulaya .
Katika mechi ya fainali dhidi ya Atletico madrid,, ronaldo ndiye aliyepiga penati ya ushindi kwa Real madrid.
 Mpaka sasa ronaldo amecheza jumla ya mechi236 na kufunga magoli 260.

       TIMU YA TAIFA YA URENO
 Katika timu ya taifa, Cristiano ronaldo amekuwa na mchango mkubwa sana, na sasa ndiye kapteni wa timu ya taifa ya ureno.
Ameiwakilisha ureno katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2006, 2010 ma 2014.
Anakumbukwa kwa kuisaidia ureno kufuzu kombe la dunia 2014, katika mechi ya mtoano dhidi ya sweeden, ambayo alifunga mabai 3 (  hat-trick) yaliyoisaidia Urenio kushinda 3-2, hivyo kupata nafasi ya kushiriki kombe la dunia 014.
Mpaka sasa ameshaichezea timu ya taifa mechi 126 na kufunga magoli 56 ( kabla ya mashindano ya EURO 2016 ).
   
   
       REKODI 5 BORA ZAIDI ZA CRISTIANO RONALDO 
  
  •     Ni mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya ( magoli 17, 2013/14)
  • Ni mchezaji mwenye hat-tricks nyingi zaidi katika msimu mmoja wa UEFA champions league ( hatricks 3, 2015/16 )
  • Ni mchezaji pekee aliyeweza kufunga zaidi ya magoli 30 kwa msimu,kwa misimu 6 mfululizo ya La liga
  • Ni mchezaji aliyefunga magoli mengi katika hatua ya makundi ya UEFA champions league ( magoli 11, 2015/16 )
  •  Ni mchezaji mwenye hat-tricks nyingi zaidi katika historia ya Real madrid ( 37)  
 
             MAISHA NJE YA SOKA
  Cristiano ronaldo pia ni balozi wa makampuni mbalimbali kama vile NIKE. Na amekuwa akifanya matangazo mbalimbali na kampuni hizo,
Pia Ronaldo ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Cristiano ronaldo jr.
  
 
  Naam ndugu msomaji , huyo ndiye Cristiano ronaldo. Ni mchezaji nyota na aliyepata mafanikio makubwa katika soka,na hiyo ndiyo safari yake kuanzia mwanzo mpaka alipofikia sasa,

      TUKUTANE KATIKA MAKALA IJAYO......AHSANTE  

Wednesday, 15 June 2016

MFAHAMU KIUNDANI LIONEL MESSI

Ndugu msomaji, karibu katika makala hii ambayo itaenda kumuelezea vizuri mchezaji bora kabisa ulimwenguni , Lionel messi.  katika makala hii  nitaenda kukujuza zaidi kuhusu nguli huyu wa mpira wa miguu ,na utaenda kumfahamu yeye ni nai, alianzia wapi na safari yake kuelekea mafanikio. Pia utajua rekodi zake mbalimbali pamoja na mafanikio yake kiujumla ikiwemo mataji na tuzo mbalmbali.....karibu twende pamoja.

  LIONEL MESSI NI NANI ?

Lionel messi ni mchezaji wa kimataifa wa argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya huko hispania, Anafahamika sana kwa jina hilo , lakini jina lake kamili ni Lionel andres messi , na alizaliwa mnamo juni 24 mwaka 1987 huko Rosario, argentina.  Alikulia na kuanza kucheza soka nchini kwao argentina katika klabu ya Newell"s old boys , mpaka alipotimiza umri wa miaka 13 ndipo alipochukuliwa na klabu ya FC Barcelona.
                                
                                                            

 MESSI ALIFIKAJE FC BARCELONA ?

katika maisha yake ya utotoni, messi alikumbwa na tat izo la upungufu wa homoni ya ukuaji, jambo ambalo lingepelekea kupunguza kasi ya ukuaji wake. kutokana na umaskini , familia yake ilishindwa kugharamia matibabu yake, lakini kipaji chake kilichoonwa na maskauti wa fc barcelona, kilisaidia kufanyika makubaliano kati ya familia yake na klabu hiyo, na hatimaye ikabidi messi aende nchini hispania kujiunga na FC Barcelona ambako angetibiwa tatizo lake pamojha na kucheza soka katika klabu hiyo , hii ilikuwa mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 13.

MAISHA YA AWALI KATIKA FC BARCELONA
Lionel messi aliingia katika akademi ya FC Barcelona ,maarufu ka,ma "La masia" ambako aliendeleza kipaji chake cha soka. Messi alizichezea timu za vijana za FC Barcelona katika ngazi zote,kwenye kipindi cha mwaka 2000 hadi 2004.
Na hatimaye mnamo oktoba mwaka 2004 alifanikiwa kuichezea kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa ya FC Barcelona. Tangia hapo aliweza kuendelea kucheza timu ya wakubwa katika misimu iliyofuatia, huku akizidi kuongeza kiwango chake .
Taratibu akaanza safari yake ya mafanikio msimu wa 2007/08, alipofanikiwa kuingia katika 3 bora katika tuzo ya mchezaji bora wa dunia , akiwa pamoja na Cristiano ronaldo na mshindi Ricardo kakla.





 MAFANIKIO MAKUBWA NDANI YA FC BARCELONA
Hatimaye baada ya kufanikiwa kuingia 3 bora ya wachezaji bora duniani katika msimu wa 2007/08 , njia ya mafanikio kwa Lionel messi ilianza kufunguka ,kwani aliendeleza makali yake na kupata mafanikio makubwa katika misimu iliyofuatia.
Alifanikiwa kunyakua kwa mara ya kwanza tuzo ya mchezaji bora wa dunia , katika msimu wa 2008/09.  Baada ya hapo messi aliweza kuibeba tena tuzo hiyo kwa mara 4 mfululizo. Hii ilikuwa katika misimu ya 2008/09 , 2009/10 , 2010/11  .na 2011/12.
Katika kipindi hicho aliisaidia FC Barcelona kushinda mataji mbalimbali kama vile ubingwa wa hispania ( la liga), kombe la uefa , kombe la mfalme na mataji mengine mengi.
Pia alifanikiwa kuweka rekodi mbalimbali kama vile kufunga magoli mengi ndani ya mwaka (91), baadhi ya rekodi hizi utaziona katika sehemu inayofuatia.
Na kata msimu wa 2014/15 , messi akishirikiana vizuri na Neymar pamoja na Luis suarez waliiwezesha FC Barcelonas kubeba makombe 3 kwa msimu ( "treble"), ukiwa ubingnwa wa ligi ,uefa na kombe la mfalme.
Hii ikamsaidia Lionel messi kushinda tena kwa mara ya 5 ,tuzo ya mchezaji bora wa dunia ( ballon d'or ), na hivyo kuweka rekodi ya kipekee kabisa.
Mpaka sasa ameichezea barcelona jumla ya mechi 563 na kuifungia magoli 464.

        

 

  TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA
Katika timu ya taifa ya argentina, messi ameicheza katika ngazi za vijana mpaka watu wazima. Alikuwepo katika kikosi cha Argentina kilichoshinda medali ya dhahabu, katika mashinndano ya olimpiki ya mwaka 2008.
Alitoa msaada kwa timu yake ya taifa pia katika masindano ya kombe la dunia na copa america. Katika mwaka 2014 aliiwezesha argentina kufika fainali ya kombe la dunia, lakini walipoteza ka kufungwa bao 1 bila.Ameweza kuchaguliwa kama mchezaji bora wa mashindano, katika kombe la dunia mwaka 2010 na 2014.
Mpaka sasa ameichezea timu ya taifa jumla ya mechi 132 na kufunga magoli 69.(haijumuishi mechi za copa america zinazoendelea sasa hivi )

                                   


   MAISHA YA KIFAMILIA
Katika upande huu , Lionel messi pamoja na mchumba wake Antonella roccuzo wamejaliwa kupata watoto 2.
Watoto hao ni TIAGO aliyezaliwa 2012 na MATEO aliyezaliwa 2015.

                                                



   
  REKODI 5 BORA ZA LIONEL MESSI
  • Ndiye mchezaji anayeongoza kwa kutwaa mara nyingi zaidi tuzo ya mchezaji bora wa dunia ( "Ballon d'or ") akiwa ameitwaa mara 5.
  • Ni mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi ndani ya mwaka mmoja ( magoli 91, mwaka 2012)
  • Ni mchezaji mwenye magoli mengi zaidi katika El clasico ( magoli 21 )
  • Ni mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga magoli 200 katika la liga. (akiwa na miaka 25)
  • ni mchezaji aliyetwaa kwa mfululizo zaidi tuzo ya Ballon d'or (mara 4)

Huyo ndiye Lionel andres messi , ambaye kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akishindanishwa na Cristiano ronaldo kutafuta mfalme wa soka wa dunia kwa sasa,
Je wewe kwa maoni yako, yupi bora kuliko mwenzake ?? usisahau kutoa maoni yako kuhusu hili.
Pia unaweza kutaja mchezaji ambaye ungependa na yeye afanyiwe uchanbuzi kama hivi, ili aweze kufahamika vizuri miongoni mwa mashabiki wa soka.
               TUKUTANE KATIKA MAKALA IJAYO.............AHSANTE.